You Are Here: Home » Resources » Sera ya Malikale

Sera ya Malikale

Suala la kutambua maana na umuhimu wa malikale kwa jamii siyo jambo geni kwa Watanzania. Tangu enzi za wahenga wetu, kabla Wazungu hawajaingilia uendeshaji wa utawala na utamaduni wa jamii zetu, wakazi wa Tanzania na kwingineko duniani walikuwa wanaenzi na kuhifadhi vitu vya kale vilivyokuwa vimejipatia umuhimu fulani kutokana na mchango wake katika jamii husika. Mathalani, sehemu zilizotumika kwa kuabudia na kutolea matambiko kama vile misitu, mapango, maporomoko ya mito na maeneo mengine ambayo jamii iliyaona kuwa yana umuhimu wa pekee, yalitunzwa vizuri sana na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Isitoshe, siyo kila mtu aliruhusiwa kuzifikia sehemu hizo, bali watu au koo chache zilizokubaliwa na jamii kwa misingi ya kihistoria ya jamii hizo. Kulitokea pia sababu zilizowafanya watu binafsi au makundi ya watu wahifadhi zana au silaha kama vile mikuki, mashoka, majembe au mavazi na kuvirithisha vitu hivyo kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Sera_ya_Malikale

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top