You Are Here: Home » Whats New » WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAKABIDHI SIMU KURIPOTI MATUKIO YA UVAMIZI WA WANYAMAPORI WAKALI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAKABIDHI SIMU KURIPOTI MATUKIO YA UVAMIZI WA WANYAMAPORI WAKALI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAKABIDHI SIMU  KURIPOTI MATUKIO YA UVAMIZI WA WANYAMAPORI  WAKALI

Kufuatia matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu kuvamia katika maeneo ya watu, Wizara ya Maliasili na Utalii leo imezindua namba maalum na kukabidhi simu (14) zitakazowezesha wananchi kupiga simu bure kwa taasisi mbalimbali za uhifadhi zilizo zinazosimamia Wanyamapori nchini chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ili kutoa taarifa juu ya uvamizi wa wanyamapori hao.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema utaratibu huo mpya utasaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka katika vituo vya karibu hasa pale matukio ya uvamizi wa wanyamapori waharibifu kama tembo yatakapotokea katika maeneo ya makazi ya watu.

“Huduma hii itawawezesha watanzania kupiga simu bure kwa mamlaka mbalimbali zinazohusika na Maliasili na Utalii kwa ajili ya kutoa taarifa za matukio ya kuvamiwa kwa wanyamapori wakali, utaratibu huu pia utasaidia kufikisha taarifa kwa haraka kwenye vituo vya utendaji na tunafanya haya kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi” amesema Dkt. Ndumbaro

Aidha, katika tukio hilo Waziri Dkt. Ndumbaro amezungumza moja kwa moja na mwananchi wa Mvomero Mkoani Morogoro ambaye ameripoti taarifa za kuvamiwa na tembo ambao wameharibu mazao yake na kuahidi kuwa tatizo hilo litashughulikiwa mara moja.

Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amesema uvamizi wa wanyamapori hao umesababisha madhara kwa wananchi ikiwemo watu kujeruhiwa na hata wengine kupoteza maisha;

“Changamoto hii ya tembo ipo kwa wananchi walio karibu na maeneo ya hifadhi ambao wamekuwa wakikumbwa na matukio ya kuvamiwa na wanyamapori hao ,kupitia zoezi hili kwetu ni faraja kubwa kwani itawasiadia wananchi kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapovamiwa na wanyama wakali hususani tembo”
amesema Mhe. Mary Masanja.

Mbali na hayo, Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Maurus Msuha amesema kama watendaji watazifanyia kazi taarifa zote ambazo zitakua zinapokewa katika vituo mbalimbali na kuzifanyia kazi kwa wakati;

“Vilio vya Wananchi vilikuwa vya muda mrefu na jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika licha ya kuwepo kwa changamoto ya Mawasiliano na wakati mwingine taarifa zilikuwa zikipelekwa sehemu ambayo siyo sahihi, lakini kupitia hili litasaidia kupata taarifa kwa haraka zaidi na wananchi watapata msaada"amesema Dkt. Msuha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema utaratibu huo mpya utasaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka katika vituo vya karibu hasa pale matukio ya uvamizi wa wanyamapori waharibifu kama tembo yatakapotokea katika maeneo ya makazi ya watu.

"Huduma hii itawawezesha watanzania kupiga simu bure kwa mamlaka mbalimbali zinazohusika na Maliasili na Utalii kwa ajili ya kutoa taarifa za matukio ya kuvamiwa kwa wanyamapori wakali, utaratibu huu pia utasaidia kufikisha taarifa kwa haraka  kwenye vituo vya utendaji na tunafanya haya kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi" amesema Dkt. Ndumbaro

Aidha, katika tukio hilo Waziri Dkt. Ndumbaro amezungumza moja kwa moja na mwananchi wa Mvomero Mkoani Morogoro ambaye ameripoti taarifa za kuvamiwa na tembo ambao wameharibu mazao yake na kuahidi kuwa tatizo hilo litashughulikiwa mara moja.

Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amesema uvamizi wa wanyamapori hao umesababisha madhara kwa wananchi ikiwemo watu kujeruhiwa na hata wengine kupoteza maisha;

"Changamoto hii ya tembo ipo kwa wananchi walio karibu na maeneo ya hifadhi ambao wamekuwa wakikumbwa na matukio ya kuvamiwa na wanyamapori hao ,kupitia zoezi hili kwetu ni faraja kubwa kwani itawasiadia wananchi kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapovamiwa na wanyama wakali hususani tembo"
amesema Mhe. Mary Masanja.

Mbali na hayo, Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Maurus Msuha amesema kama watendaji watazifanyia kazi taarifa zote ambazo zitakua  zinapokewa katika vituo mbalimbali na kuzifanyia kazi kwa wakati;

"Vilio vya Wananchi vilikuwa vya muda mrefu na jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika licha ya kuwepo kwa changamoto ya Mawasiliano na wakati mwingine taarifa zilikuwa zikipelekwa sehemu ambayo siyo sahihi, lakini kupitia hili litasaidia kupata taarifa kwa haraka zaidi na wananchi watapata msaada"amesema Dkt. Msuha

© 2021 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top