You Are Here: Home » Whats New » WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUANDAA MWONGOZO WA KUTUNZA NA KUTEKETEZA KUMBUKUMBU

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUANDAA MWONGOZO WA KUTUNZA NA KUTEKETEZA KUMBUKUMBU

WIZARA  YA MALIASILI NA UTALII KUANDAA MWONGOZO WA KUTUNZA NA KUTEKETEZA KUMBUKUMBU

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prisca Lwangili  leo tarehe 2 Agosti, 2022 amefungua kikao kazi cha kuandaa Mwongozo wa Kutunza na Kuteketeza Kumbukumbu za wizara kwa maafisa wa Idara na vitengo kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara   Swagaswaga Jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho Lwangili amesema  mwongozo huo utawasaidia Watumishi kutunza vizuri kumbukumbu zilizochujwa na kutambuliwa  kwa lengo la  kuepusha kuvuja kwa siri za serikali sambamba na kuziharibu kumbukumbu  ambazo hazijasajiliwa lakini zina taarifa muhimu kwa wizara na Taifa kwa ujumla.

Aidha, katika kikao  hicho Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu amewakumbusha Watumishi kuendelea kutunza siri za serikali kwa maslahi mapana ya taifa.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top