You Are Here: Home » Whats New » WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DKT. NDUMBARO AIAGIZA TFS KUPANDA MITI ASILI KATIKA BWAWA LA UMEME

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DKT. NDUMBARO AIAGIZA TFS KUPANDA MITI ASILI KATIKA BWAWA LA UMEME

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DKT. NDUMBARO AIAGIZA TFS KUPANDA MITI ASILI KATIKA BWAWA LA UMEME

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kuanza kupanda miti ya asili katika maeneo ambayo yako wazi na hayataguswa na Ujenzi unaoendelea wa Bwawa la Julius Nyerere ( JNHPP-MW2115)

Ametoa rai hiyo juzi wakati alipotembelea maeneo ya Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere hususani kukagua eneo ambalo Wizara ya Maliasili na Utalii imepewa jukumu la kung’oa miti ili kusafisha eneo kwa ajili ya kutengeneza Bwawa, kazi inayofanywa na JWTZ wakishirikiana na Wizara hiyo.


Amesema anataka kuona miti ya asili inarudishiwa katika maeneo hayataguswa na ujenzi huo licha ya kuwa yameathirika kutokana na ujenzi wa mradi huo


” Nataka kuona miti ile ile ya asili inarudishiwa msije mkaribu kuipanda ile miti ya kule Shamba la Miti Sao Hill ile iacheni kule kule ndiko eneo lake huku pandeni ya asili” alisisitiza Dkt.Ndumbaro.


Katika hatua hiyo, Dkt.Ndumbaro ameitaka TFS kuanza mara moja kuotesha vitalu vya miche ya miti ya asili kwa kutumia Wataalamu wake ili kukimbizana na muda.


Amesema ni vyema zoezi hilo likaanza mapema kwa vile miti ya asili inakuwa kwa taratibu sana, Hivyo mara baada ya hatua za ujenzi wa mradi huo kukamilika nayo miti iwe tayari imeshakua


Katika hatua nyingine, Dkt.Damas Daniel Ndumbaro amesema kwa hatua ulikofikia   Ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere licja ya kupigwa vita ndani na nje ya nchi kwa sasa hakuna wa kuupinga tena

 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amesema maeneo ambayo yanauzunguka mradi huo yataendelea kutumika kwa ajili ya shughuli za kiutalii kwa vile madhari ya Bwawa lenyewe inahamasisha shughuli za utalii.


Aidha, Amesema eneo hilo la Bwawa litaendelea kuhifadhiwa kama eneo lingine la Hifadhi kwa kupanda miti zaidi ili kulinda vyanzo vya maji katika maeneo hayo.

 

© 2021 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top