You Are Here: Home » Whats New » WAZIRI NDUMBARO KUONGOZA WATU 300 KUFIKA KILELENI MT.KILIMANJARO

WAZIRI NDUMBARO KUONGOZA WATU 300 KUFIKA KILELENI MT.KILIMANJARO

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro ametangaza watu 300 wanatarajia kupanda Mlima Kilimanjaro mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 21, 2021 jijini Arusha, Waziri Ndumbaro amesema mwaka huu kutakuwa na maandalizi ya aina yake kuhakikisha wanaojitokeza wanafika kileleni.

Waziri Ndumbaro amewataka Watanzania kuendelea kujiandikisha kupanda Mlima huo ili kuweka historia ya kushiriki miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika.

Amesema Kampuni ya Utalii ya Zara ndio itashirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kupandisha watalii Mlima Kilimanjaro ambapo gharama itakuwa ni Sh800, 000.

Amesema hadi kufikia leo watanzania 120 wamejitokeza huku nafasi zilizopo zikiwa za watu 300 na zoezi la kupanda mlima huo litaanza Desemba 5 mwaka huu.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top