WAZIRI CHANA AFUNGUA MKUTANO WA WABUNGE WA AFRIKA

Wabunge zaidi ya 22 kutoka nchi 14 za Afrika, wamekutana nchini Tanzania kujadili masuala ya ulinzi na amani hasa katika kipindi hiki cha janga la UVIKO 19 ulioandaliwa na Parliamentarians for Global Action (PGA)

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akifungua rasmi mkutano huo ameeleza kuwa ujio wa Wabunge hao ni matokeo chanya ya juhudi za Tanzania kuvitangaza vyema vivutio vya Utalii.
Waziri Chana amezitaka Taasisi za Umma na za Binafsi zinazo shughulika na Utalii ziendelee kuboresha huduma ili ziweze kwenda na ongezeko la watalii watakaoingia nchini baada ya kuzinduliwa kwa Filamu ya Royal Tour.
“Tunatarajia wenzetu wa Viwanja vya ndege wamejiandaa vyema, sekta ya mawasiliano,hoteli zetu, waongoza watalii, Mama lishe, wafugaji, wakulima na wote watakuwa wamejianda vyema katika utoaji wa huduma za kiwango cha juu” Amesema Mhe. Chana
Waziri Chana amewakaribisha Wabunge hao na ugeni walioambatana nao watembelee maeneo ya Utalii kabla ya kuondoka nchini ili nao waonje uzuri wa Tanzania.