You Are Here: Home » Whats New » UZINDUZI WA MKAKATI WA KITAIFA WA KUSIMAMIA UTATUZI WA MIGOGORO BAINA YA BINADAMU NA WANYAMAPORI

UZINDUZI WA MKAKATI WA KITAIFA WA KUSIMAMIA UTATUZI WA MIGOGORO BAINA YA BINADAMU NA WANYAMAPORI

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye idadi kubwa ya wanyamapori na imetenga zaidi ya theluthi ya ardhi yake kwa ajili ya uhifadhi wa Wanyamapori. Ardhi hiyo ni Hifadhi za Taifa 22, Mapori ya Akiba 22, Mapori Tengefu 30, Maeneo ya Ardhioevu matatu na Maeneo 38 ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori za Jamii. Tanzania inaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori jamii ya paka wakiwemo simba na chui na nchi ya tatu kwa idadi ya tembo duniani. Hii ni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa katika shughuli za uhifadhi wanyamapori hao, huku tukithamini mchango mkubwa unaotolewa na jamii zinazozunguka maeneo ya Hifadhi.

HOTUBA YA MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA (MB), WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII WAKATI WA UZINDUZI WA MKAKATI WA KITAIFA WA KUSIMAMIA UTATUZI WA MIGOGORO BAINA YA BINADAMU NA WANYAMAPORI, UKUMBI WA KILIMANJARO, JENGO LA HAZINA, DODOMA, TAREHE 08 OKTOBA 2020.

Dkt. Aloyce K. Nzuki, Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii;
Dkt. Allan H. Kijazi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii;
Dkt. Maurus J. Msuha, Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori;
Makamishna wa Uhifadhi wa TAWA, TANAPA, NCAA na TFS;
Wakuu wa Taasisi za Utafiti na Mafunzo, TAWIRI, MWEKA, Pasiansi na Likuyu Sekamaganga;
Wawakilishi wa wadau wa maendeleo USAID, GIZ, na UNDP;
Wawakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali PAMS, WWF, WCS, FZS, STEP, OIKOS, Grumet Fund na RESOLVE;
Wawakilishi wa wakulima na wafugaji kutoka sehemu mbalimbali;
Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii;
Waandishi wa Habari;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kuhudhuria katika hafla hii muhimu ya uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Utatuzi wa Migogoro Baina ya Binadamu na Wanyamapori. Kufika kwenu kunadhihirisha dhamira ya dhati ya kutafuta suluhu ya migogoro baina ya wanyamapori na binadamu, hivyo ninawashukuru na kuwapongeza sana.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, 

Wanyamapori waliohifadhiwa katika maeneo hayo ni kivutio kikubwa cha utalii na ni rasilimali muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi na maendeleo ya jamii. Sote tunafahamu kuwa, utalii unachangia zaidi ya asilimia 25 ya fedha za kigeni na hivyo uhifadhi wa rasilimali hizi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, 
Kwa muda mrefu binadamu na wanyamapori wamekuwa wakiishi pamoja kwa kutegemeana. Hata hivyo, kuongezeka kwa idadi ya watu na mifugo; mabadiliko ya tabia nchi; na kupanuka kwa shughuli za kibinadamu hasa makazi na kilimo kusikozingatia matumizi bora ya ardhi kumesababisha migogoro baina ya binadamu na wanyamapori. Migogoro hiyo inatokana na kujeruhiwa au kuuawa kwa watu, kuuawa kwa mifugo, uharibifu wa mazao na mali nyingine.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Katika kukabiliana na migogoro hiyo, Wizara imetekeleza yafuatayo:
1. Imetambua migogoro baina ya binadamu na wanyamapori kama tatizo mtambuka la kiuhifadhi na kuliingiza katika Sera ya Wanyamapori ya mwaka 2007 na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya 2009;
2. Imeweka utaratibu wa kulipa kifuta jasho na machozi kwa wahanga wa matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu ikiwa ni utekelezaji wa Kanuni za Kifuta Jasho na Machozi za mwaka 2011. Kwa mfano, katika kipindi cha mwaka 2015/16 hadi 2018/19 jumla ya TZS 5,982,285,050.00 zimelipwa kama kifuta jasho na machozi;
3. Imetunga Kanuni za Usimamizi wa Shoroba na Maeneo ya Mtawanyiko wa Wanyamapori za mwaka 2018. Kanuni hizi zinasimamia wanyamapori katika maeneo yenye mwingiliano mkubwa na wananchi;
4. Imeendelea kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na migogoro baina ya wanyamapori na binadamu, hususan kwa jamii zinazoishi kandokando ya hifadhi;
5. Imefanya doria 29,590 za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu. Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 jumla ya wanyamapori wakali 547 walidhibitiwa baada ya kuhatarisha maisha ya wananchi; na
6. Inaendelea kushirikiana na wahisani katika kutekeleza miradi ya matumizi ya mbinu shirikishi za kupambana na wanyamapori wakali na waharibifu. Miradi hiyo ni ujenzi wa maboma salama katika jamii za kimasai, matumizi ya pilipili “chilly bombs”, uwekaji wa matuta katika maeneo yenye uvamizi mkubwa kuzuia wanyamapori kuvuka kwenda mashambani;

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, 

Katika kutafuta suluhu endelevu na kwa kuzingatia umuhimu wa kutatua changamoto ya migongano kati ya wanyamapori na binadamu, Wizara imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Utatuzi wa Migogoro Baina ya Binadamu na Wanyamapori. Mkakati huu unalenga yafuatayo:
1. Kuwezesha jamii kutumia mbinu shirikishi na zisizokuwa na madhara kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu;
2. Kupunguza madhara ya kuishi na wanyamapori;
3. Kuongeza uwezo wa Wizara katika kukabiliana na matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu;
4. Kuhimiza matumizi bora ya ardhi, hasa katika maeneo ya shoroba na maeneo ya mtawanyiko wa wanyamapori;
5. Kutoa elimu kwa jamiii kuhusu namna bora ya kusimamia utatuzi wa migogoro baina ya binadamu na wanyamapori;
6. Kutumia rasilimali zilizopo katika kutatua migogoro kwa kuzingatia maeneo yaliyoathirika zaidi;
7. Kufanya utafiti ili kufahamu namna bora ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu; na
8. Kushirikisha jamii katika usimamizi wa maeneo ya shoroba na mtawanyiko wa wanyamapori.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, 
Katika kutekeleza Mkakati Wizara itafanya mambo yafuatayo:
1. Itaanzisha Kitengo cha Utatuzi wa Migogoro Baina ya Binadamu na Wanyamapori. Kitengo hicho kitapewa mafunzo maalumu kukiwezesha kufundisha jamii njia bora za kutatua migogoro baina ya binadamu na wanyamapori;
2. Itaanzisha kanzidata ya kitaifa kwa ajili ya kukusanya, takwimu za matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu;
3. Itawezesha timu za TAWA, TANAPA, NCAA na Askari wa Vijiji kukabiliana na matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa haraka pale yanapotokea;
4. Kuanzisha line maalum za simu “Hotline” kwa kila kanda kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa taarifa na kuongeza ufanisi wa kuzifanyia kazi;
5. Kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kuweka suala la migogoro baina ya binadamu na wanyamapori katika mitaala ili lifundishwe kuanzia shule za awali, msingi na sekondari;
6. Itashirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kuunda Kamati ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ya Kusimamia Mwingiliano wa Watu na Wanyamapori (Multi-sectoral Human-Wildlife Coexistence Land Use Planning Committee); na
7. Itaweka utaratibu wa wanafunzi kutembelea hifadhi za wanyamapori ili kuwajengea hamasa ya uhifadhi na kutembelea vivutio vya Utalii.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, 
Utekelezaji wa Mkakati huu unategemea kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa rasilimali fedha na watu pamoja na matumizi ya teknolojia. Hivyo, ninawaomba:
1. Wadau wa maendeleo, Asasi Zisizo za Kiserikali na watu binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza Mkakati huu.
Tayari tumetaarifiwa hapa na Katibu Mkuu kuwa, wapo wadau waliojitokeza kufanikisha utekelezaji wa Mkakati huu ambao ni GIZ, WWF, TPW na PAMS Foundation. Naomba nitangulize shukrani zangu za dhati kwa mashirika haya na niendelee kuwasihi wadau wengine kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara katika utekelezaji wa Mkakati huu;
2. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi;
Aidha, ninaelekeza yafuatayo:
1. Taasisi za uhifadhi (NCAA, TANAPA, TAWA na TFS) chini ya mfumo wa Jeshi la Uhifadhi zishirikiane katika kutekeleza Mkakati huu;
2. Kuundwa Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Matukio “Rapid Response Team”. Kikosi hiki kitakuwa msaada mkubwa katika kuokoa mali na maisha ya binadamu dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu.
3. Mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa taarifa za wanyamapori wakali na waharibifu ukamilishwe kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2020/2021;
4. Utaratibu wa kutenga maeneo ya shoroba na mtawanyiko wa wanyamapori uharakishwe;

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, 
Natambua maandalizi ya mkakati kama huu ulihitaji rasilimali watu na fedha. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kukamilisha maandalizi ya Mkakati huu ambao ninauzindua leo. Kipekee niwashukuru USAID kupitia mradi wa PROTECT; GIZ na Wizara yangu kwa kufadhili maandalizi ya Mkakati na uzinduzi wake. Naomba nitumie fursa kuwaomba wadau mlioko hapa na wale ambao hawapo hapa kufadhili utekelezaji wa Mkakati huu. Kwa Taasisi za Wizara (TANAPA, NCAA, TAWA na TFS) naelekeza mtenge bajeti katika kutekeleza Mkakati huu. Aidha, niwashukuru wataalam waliofanikisha kazi hii wakiongozwa na Dkt. Trevor Jones na Wizara yangu kupitia kwa Katibu Mkuu Dkt. Aloyce Nzuki, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Allan Kijazi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha kwa kuratibu zoezi zima la uandaaji wa Mkakati huu. Mwisho niishukuru kamati ya maandalizi kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa hafla ya uzinduzi inafanikiwa.

Baada ya kusema hayo, sasa naomba kutamka rasmi kuwa Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Utatuzi wa Migogoro Baina ya Binadamu na Wanyamapori umezinduliwa rasmi.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Hotuba_ya_Waziri_08_Oktoba_2020_-1

© 2020 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top