You Are Here: Home » Whats New » UZINDUZI WA MATANGAZO YA VIVUTIO VYA UTALII KATIKA MABASI NCHINI ISRAEL

UZINDUZI WA MATANGAZO YA VIVUTIO VYA UTALII KATIKA MABASI NCHINI ISRAEL

UZINDUZI WA MATANGAZO YA VIVUTIO VYA UTALII KATIKA MABASI NCHINI ISRAEL

Katika kuhitimisha maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mhe. Job Daudi Masima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Israel amezindua matangazo ya vivutio vya utalii katika mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kati ya jiji la Tel Aviv na miji ya jirani, katika stendi kuu ya mabasi, katika kitongoji cha Petach Tikva.

Matangazo hayo yamebandikwa kwenye mabasi yapatayo 125 kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe 10 - 31 Disemba 2021. Matangazo hayo yanayoonesha Mlima Kilimanjaro; Wanyama katika hifadhi ya Serengeti; Ngorongoro na fukwe za Zanzibar yanatoa fursa kwa wakazi wa Israel kujionea vivutio hivyo na kuhamasika kutembelea Tanzania mara baada ya masharti ya UVIKO kulegezwa.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top