You Are Here: Home » Whats New » UWANJA WA NDEGE WA NDULI KUWA LANGO LA FURSA YA UTALII.

UWANJA WA NDEGE WA NDULI KUWA LANGO LA FURSA YA UTALII.

UWANJA WA NDEGE WA NDULI KUWA LANGO LA FURSA YA UTALII.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli mkoani Iringa utakapokamilika utaongeza fursa za kibiashara na kuifungua zaidi kanda ya Kusini kwenye sekta ya Utalii.

Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo Agosti 12, 2022 mkoani Iringa alipokuwa akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli na akitoa rai kwa wananchi wajipange katika kuchangamkia fursa zitakazoletwa na uwanja huo katika sekta ya Utalii

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili ja Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana licha ya kupongeza jitihada hizo za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan za kuendelea kufungua milango ya Utalii nchini amesema uwanja huo utaongeza idadi ya Watalii kwenye vivutio vya Kanda ya Kusini, kuongeza hamasa kwa wawekezaji na chachu katika biashara ya mazao ya misitu pamoja na usafirishaji wa vyakula kwenye mikoa mingine yenye Idadi kubwa ya Watalii.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top