UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA MISITU TANZANIA (TaFF)
.jpg)
Kufuatia Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Prof. Shabani Athumani Chamshama kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb) kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 79(4) cha Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF): -
1. Dkt. Tuli Salum Msuya, Katibu wa Mfuko wa Misitu (TaFF), Wizara ya Maliasili na Utalii, Dodoma.
2. Prof. Dos Santos Aristariki Silayo, Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
3. Prof. Yonika Mathew Ngaga, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Morogoro.
4. CPA. Christina F. Mongi, Meneja Ukaguzi, Kampuni ya Ukaguzi Innovex, Dar es Salaam.
5. Bi. Felista Steven Lelo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dodoma.
6. Bibi Lulu Ng’wanakilala, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uwakili ya Legal Service Facility (LSF), Dar es Salaam.
7. Eng. Enock Nyanda Emmanuel, Mkurugenzi Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dodoma.
8. Dkt. Revocatus Petro Mushumbusi, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Morogoro.
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 02 Septemba, 2022 hadi 1 Septemba, 2025