You Are Here: Home » Whats New » UTALII WA SOKWEMTU KUANZISHWA KATIKA HIFADHI YA TAIFA RUMANYIKA NA IBANDA MKOANI KAGERA

UTALII WA SOKWEMTU KUANZISHWA KATIKA HIFADHI YA TAIFA RUMANYIKA NA IBANDA MKOANI KAGERA

Serikali imesema itawapandikiza Sokwemtu katika hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu na Ibanda mkoani Kagera kwa kuwa hifadhi hizo zina Ikolojia na chakula cha kutosha kinachoruhusu kustawi kwa wanyamapori hao hatua itakayochangia kukuza shughuli za utalii wa Sokwemtu hapa nchini na kuongeza pato la Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kukagua maendeleo ya shughuli za uhifadhi katika hifadhi hizo zilizotangazwa hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, mkoani Kagera.

Dkt. Kigwangalla amesema mpango huo umekuja kufuatia taarifa za kitaalam zinaonesha kwamba katika miaka mingi iliyopita kulikua na Sokwemtu katika maeneo hayo ya wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambayo watalaam wanasema ikolojia yake inaruhusu kustawi kwa wanyamapori hao kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.

Amesema mpango huo hautahusisha upandikizaji wa wanyamapori wote kwa kuwa kazi hiyo itazingatia matokeo ya tafiti za kitaalam zitakazofanyika kwanza ili kujua Ikolojia ya eneo hilo inaruhusu wanyama wa aina gani wanaoweza kuishi.

“Sasa hivi tuna taarifa kwamba katika miaka mingi iliyopita kulikua na Sokwemtu katika hifadhi hizi na katika eneo lote hili la wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambayo watalaam wanasema ikolojia yake inakwenda moja kwa moja mpaka kwenye milima ya Rwenzori yenye wanyama hawa nchini Uganda” Amesema Dkt. Kigwangalla.

Amefafanua kuwa kazi inayoendelea sasa katika maeneo hayo ni kuendeleza shughuli za uhifadhi katika ili kulinda mandhari nzuri iliyopo ikiwemo milima mizuri, miinuko na mabonde yaliyoko kwenye hifadhi hizo ambayo ni kivutio kizuri cha utalii.

Aidha, amebainisha kuwa kwa sasa Wizara imejikita zaidi katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo hayo kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi waitembelee Tanzania akitoa wito kwa wananchi wanaoishi kuzunguka hifadhi hizo kuitumia fursa hiyo kunufaika kiuchumi kwa kutangaza utamaduni wao, vyakula vyao, maisha yao, ngoma zao na lugha yao hatua itakayosababisha baadhi ya wageni kutoka nchi za nje kuchagua kuja kuishi kwenye familia hizo kwa lengo la kujifunza utamaduni wao.

Kuhusu elimu kwa umma na ushiriki wa wananchi kushiriki katika uchumi mpana wa kiutalii Dkt. Kigwangalla amesema Wizara na wahifadhi wamekuwa wakiwaelimisha wananchi kupitia shughuli za kiutamaduni, kujiandaa kupokea wageni, kutumia fursa ya kuuza vitu kwenye hoteli za kitalii zilizoko kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na wananchi kujiandaa kutenga maeneo yao kwa ajili ya uhifadhi.

“Mbali na kuwatumia askari wa wanyamapori ambao wamekuwa na kazi kubwa ya kuwarudisha wanyamapori kwenye maeneo yao pindi wanapotoka nje ya hifadhi, tunawaelimisha wananchi wanaoishi kuzunguka hifadhi zetu namna bora ya kuishi pamoja na wanyamapori ili wajue vitu gani wafanye na wasivyotakiwa kufanya wanapokutana na wanyamapori pia matumizi ya mbinu za kisayansi ambazo zimekuwa zikitumika ikiwemo kuweka mizinga katika maeneo ya mipaka ili kuwazuia wanyama kama Tembo kuingia katika maeneo ya makazi”

Ametoa wito kwa wananchi wanaoishi katika maeneo kuzunguka hifadhi kujenga nyumba zao mbali na kuacha eneo la kutosha ili kuwezesha wanyamapori kudhibitiwa kirahisi na askari wa wanyamapori pindi wanapoanza kutoka katika maeneo ya hifadhi.

Kuhusu uboreshaji wa miundombinu katika maeneo ya hifadhi Dkt. Kigwangalla amesema kuna mipango ya maendeleo ya hifadhi na mradi mkubwa unaotarajiwa kutekelezwa katika hifadhi mpya tano pamoja na hifadhi ya Taifa ya Serengeti unaofadhiliwa na Benki ya Maendelep ya Afrika ambapo Tanzania itapata zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 100 ambazo zitajenga miundombinu mbalimbali ikiwemo madaraja, viwanja vya ndege, barabara za watalii na barabara za doria pamoja na misaada inayotolewa katika jamii.

“Kazi kubwa zinatarajiwa kufanyika katika hifadhi hizi na ndio maana tunakuja mara kwa mara katika maeneo haya ili kuyaelewa maeneo haya, kujifunza changamoto zilizopo pamoja na kuziwekea mikakati ya kuzitafutia ufumbuzi” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande wa vita dhidi ya Ujangili ameeleza kuwa Serikali haitarajii wananchi wajihusishe na vitendo vya ujangili kwa kuwa suala hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria akibainisha kwamba Serikali ya awamu ya tano imeweka mifumo madhubuti ya kushughulikia vitendo vya ujangili.

Amesisitiza kwamba Serikali kwa sasa imejikita katika kuzungumzia biashara na namna bora ya kukuza biashara na kufaidisha wananchi wananchi kuzunguka maeneo ya hifadhi.

“Mtu yeyote akifanya ujangili tutamkamata tu, hatutarajii wananchi wajihusishe na ujangili, mtu akifanya ujangili awe ndani ya hifadhi au akiwa huko uraiani tutamkamata tu, katika Serikali ya awamu ya tano tumefanikiwa kudhibiti ujangili, tumeweka mifumo madhubuti ya kudhibiti ujangili. Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande wake Kamishna mwandamizi wa uhifadhi Kanda ya Magharibu (TANAPA) Bw. Martin Loibooki ameeleza kuwa hifadhi ya Ibanda ina wanyamapori tofauti tofauti wakiwemo nyati, swala na wanyama wengineo.

Ameeleza kuwa katika miaka ya nyuma hifadhi hiyo ilivamiwa na wakimbizi na watu wengine waliokuwa wanafanya uharibifu mbalimbali hali iliyosababisha wanyama wengi kupungua na wengine kutoweka.

“Mpango wa TANAPA kwa sasa ni kuwarudisha wanyama waliootoweka kwa sasa, ulinzi umeimarika na ndio maana tunaona uoto wa asili umerudia katika hali yake ya kawaida kutokana na kuimarika kwa ulinzi” Amesisitiza

Akitoa ufafanuzi kuhusu hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu amesema kuwa hifadhi hiyo imejaa uoto wa asili,milima na misitu ina vivutio mbalimbali yakiwemo maziwa na uoto wa asili wa miyi

Kuhusu hifadhi ya Taifa Ibanda amesema kuwa hifadhi hiyo inapakana na Rwanda na   Uganda na ina miti aina ya migunga ambayo ni kivutio na chakula cha Twiga  

Naye Kamishana Msaidizi wa Uhifadhi anayesimamia hifadhi hizo, M.B Moronda ameeleza kuwa mikakati ya kuboresha miundombinu ya hifadhi hizo kwa lengo la kuzifungua ili kuruhusu watalii kuanza kuzitembelea hifadhi hizo na kutangaza utalii.

“Tumeanza kupata maombi ya watu kutoka nchini Uganda wanaotaka kuja kutalii baada ya kusikia hifadhi hizo zimetangazwa kuwa Hifadhi za Taifa.

© 2020 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top