You Are Here: Home » Whats New » UKAGUZI WA WAKALA WA BIASHARA ZA UTALII NCHINI

UKAGUZI WA WAKALA WA BIASHARA ZA UTALII NCHINI

UKAGUZI WA WAKALA WA BIASHARA ZA UTALII NCHINI

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwajulisha wafanyabiashara za utalii nchini kuwa, ukaguzi wa wakala wa biashara za utalii unatarajiwa kufanyika katika malango ya kuingilia wageni ya Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwajulisha wafanyabiashara za utalii nchini kuwa, ukaguzi wa wakala wa biashara za utalii unatarajiwa kufanyika katika malango ya kuingilia wageni ya Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

Ukaguzi huo kwa Wakala wa biashara za utalii nchini ni wa kawaida na unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Utalii Na. 29 ya mwaka 2008 kwa lengo la kubaini wakala wa biashara za utalii wanaoendesha biashara zao kinyume cha Sheria pamoja na kutoa elimu kuhusu kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia biashara za utalii nchini. 

Aina za biashara au shughuli za utalii zinazokaguliwa zinahusisha Wakala wa Usafirishaji Watalii (Tour Operators), Waongoza Watalii (Tour Guides), watoa huduma za malazi na watoa huduma za kukodisha magari kwa shughuli za utalii (Car Rental or Hire).

 

Wizara inatumia  fursa hii kuwakumbusha wakala wote wa biashara za utalii wasiolipa Leseni ya Biashara za Utalii (TTBL) kulipia kupitia mfumo wa kielektroniki wa Wizara, MNRT – Portal unaopatikana katika tovuti ya Wizara ya Maliasili na Utalii  https://portal.maliasili.go.tz/#!/  ili kuepuka usumbufu wowote unaoweza kujitokeza.
    
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu www.maliasili.go.tz au fika kwenye Ofisi zetu za Makao Makuu zilizopo Dodoma au Ofisi za Utalii za Kanda zilizopo Jengo la Mpingo- Dar es Salaam, Jengo la NSSF - Iringa, TANAPA Makao Makuu – Arusha na Ofisi ya Utalii Kanda ya Ziwa – Mwanza.

 

Imetolewa na; -

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

UKAGUZI_WA_WAKALA_WA_BIASHARA_ZA_UTALII_NCHINI_-_final

© 2023 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top