You Are Here: Home » Whats New » UAMUZI WA SERIKALI KUHUSU KUENDELEA KWA UVUNAJI, USAFIRISHAJI NA BIASHARA YA MAZAO NA BIDHAA ZA MTI

UAMUZI WA SERIKALI KUHUSU KUENDELEA KWA UVUNAJI, USAFIRISHAJI NA BIASHARA YA MAZAO NA BIDHAA ZA MTI

Mti jamii ya Mkurungu (Pterocarpus tinctorius) ambao pia unafahamika kwa jina la ‘Mkula’ huko Zambia, ni mojawapo ya jamii (species) za miti ambayo hupatikana kwa wingi nchini katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Mbeya na Rukwa. Aidha, miti hii hupatikana pia katika nchi jirani ikiwemo DRC Kongo, Zambia na Msumbiji.

Hapa nchini, miti hii hutumika kwa kiwango kidogo katika eneo la ujenzi na kutengenezea samani ikilinganishwa na miti mingine kama Mninga, Mkongo au Mkangazi. Hii ni kutokana na tabia yake ya kupindapinda na kuwa na kimo kifupi cha kuweza kutoa ubao mrefu hususani ile inayopatikana katika ikolojia kame ya miombo barani Afrika, kama nchini Zambia na pia hapa Tanzania kwa baadhi ya sehemu za mikoa ya Katavi, Mbeya na Rukwa. Kwa miti inayopatikana katika ikolojia ya miombo yenye unyevunyevu kiasi (wet miombo woodlands), miti hii inaweza kuwa na tabia za uimara (properties) zinazoshabihiana na miti ya Mninga, Mvule, Mkangazi na Mkongo.

Mazao ya mti huu wa mkurungu yalipata umaarufu sana katika soko la nje hususani nchini China katika miaka ya 2000. Taarifa zinaonesha mti huu unaweza kutumika kwa kutengenezea samani mbalimbali. Aidha, matumizi yake hutegemea sana kiwango cha teknolojia ya uchakataji mbao (wood engineering) kama ilivyo kwa baadhi ya nchi barani Asia hususani China. Kutokana na uwezo huo wa kiteknolojia, China imekuwa ikinunua miti hii kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwemo Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Msumbiji na pia Tanzania. Kutokana na kuimarika kwa soko la nje, kulipelekea kukua na kushamili kwa soko la mti huu hapa nchini siku hadi siku.

Kwa taarifa zaidi pakua .......

PRESS_RELEASE-_MKURUNGU

© 2021 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top