You Are Here: Home » Whats New » TANZANIA YASISITIZA UHIFADHI WA MIOMBO MKUTANO WA KIMATAIFA WA KIKANDA MSUMBIJI.

TANZANIA YASISITIZA UHIFADHI WA MIOMBO MKUTANO WA KIMATAIFA WA KIKANDA MSUMBIJI.

TANZANIA YASISITIZA UHIFADHI WA MIOMBO MKUTANO WA KIMATAIFA WA KIKANDA MSUMBIJI.

Tanzania imetoa wito kwa nchi zote za Bara la Afrika kuhakikisha kuwa zinaongeza nguvu katika kuhifadhi rasilimali za misitu ya miombo ambayo ni muhimu kwa maisha ya Waafrika na Dunia kwa Ujumla.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana alipokua akizungumza katika Mkutano wa kwanza wa Kikanda kuhusu Usimamizi Endelevu wa Misitu ya Miombo unaoendelea Jijini Maputo nchini Msumbiji ukihudhuriwa na viongozi wa juu wa Kisekta kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika.
Akizungumza katika mkutano huo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema nchi za Afrika zinapaswa kuendelea kujadili kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa misitu ya miombo na kuweka mikakati endelevu ya kulinda rasilimali hiyo muhimu kwa Bara la Afrika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top