You Are Here: Home » Whats New » Tanzania Kuwa Mwenyeji wa Warsha ya Kimataifa ya Takwimu za Utalii

Tanzania Kuwa Mwenyeji wa Warsha ya Kimataifa ya Takwimu za Utalii

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Warsha ya kimataifa ya takwimu za utalii ambayo itafanyika kwa siku nne , tarehe 18 hadi 21 mwezi huu, katika ukumbi wa Benki Kuu Dar es Salaam.

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA WARSHA YA KIMATAIFA YA

TAKWIMU ZA UTALII

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Warsha ya kimataifa ya takwimu za utalii ambayo itafanyika kwa siku nne , tarehe 18 hadi 21 mwezi huu, katika ukumbi wa Benki Kuu Dar es Salaam.

Warsha hiyo ambayo imeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) na Shirika la Utalii la Nchi za Kusini mwa Afrika (RETOSA) ni sehemu ya utekelezaji wa  mpango wa UNWTO wa Takwimu (Joint National Statistical Capacity Building Programme – NSCBP)

Kwa kutambua kuwa, nchi wanachama zimepiga hatua mbalimbali tofauti katika kuendeleza mifumo yao binafsi ya takwimu za utalii, katika warsha hii wataalam watabadilishana uzoefu kuhusu vipimo bora vya takwimu, tathmini, na mikakati ya usimamizi wa sekta ya utalii. Hii itasaidia taasisi zinazohusika katika nchi wanachama wa RETOSA kuimarisha mifumo yao ya takwimu mbalimbali zinazohusiana na utalii.

Watakaohudhuria warsha hii ni wachumi, wataalamu wa takwimu, watafiti na wataalamu wa sekta ya utalii kutoka taasisi mbalimbali za utalii, Benki Kuu, Ofisi za takwimu, Wizara mbalimbali na wadau wengine husika.

Warsha itakayofanyika Tanzania itakuwa ni ya nne katika mfululizo wa warsha za Takwimu za Utalii katika nchi wanachama wa RETOSA. Awali zilifanyika Victoria falls Zimbabwe December 2011, Masvingo Zimbabwe May 2012 na Ezulwini Valley Swaziland September 2012

[MWISHO]

George Matiko

MSEMAJI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

15 Machi  2013

SIMU 0784 468047

© 2021 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top