You Are Here: Home » Whats New » TANZANIA KUTUMIA FURSA YA KOMBE LA DUNIA 2022 KUTANGAZA UTALII

TANZANIA KUTUMIA FURSA YA KOMBE LA DUNIA 2022 KUTANGAZA UTALII

TANZANIA KUTUMIA FURSA YA KOMBE LA DUNIA 2022 KUTANGAZA UTALII

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka amefanya ziara ya kikazi nchini Qatar kwa lengo la kuweka mikakati ya kutumia fursa ya Mashindano ya Kombe la Dunia 2022 kutangaza utalii wa Tanzania.

Prof. Eliamani Sedoyeka amekutana na kufanya mazungunzo na Waandaaji wa tukio la African Village ambalo litakuwa linatangaza utalii wa nchi mbalimbali wakati wa Mashindano ya kombe la Dunia nchini Qatar yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 20 Novemba hadi 18 Desemba 2022.

Mbali na fursa hiyo ya kutumia Mashindano ya Kombe la Dunia 2022 kutangaza Vivutio vya Utalii vya Tanzania Prof. Sedoyeka amekutana na wadau mbalimbali kuhamasisha na kuelezea fursa za uwekezaji zilizo katika Sekta ya Utalii nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Felix John na Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bi. Hafsa Mbamba.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top