You Are Here: Home » Whats New » WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA MWAKA 2017

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA MWAKA 2017

Wizara ya Maliasili na Utalii inawakaribisha wananchi wote kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar–es-Salaam (Sabasaba) yatakayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa kuanzia tarehe 28 Juni hadi 8 Julai 2017. Karibu ujionee shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa katika Maonesho ya mwaka huu kutakuwa na kiingilio kwa wale watakaopenda kutembelea Bustani ya wanyamapori.

Kiwango cha tozo kitakuwa shilingi 1,000/= kwa watu wazima na shilingi 500/= kwa watoto. Watoto walio chini ya miaka mitano wataingia bure. Gharama hizo za viingilio ni kwa ajili ya kuchangia gharama za utunzaji wa Wanyamapori hai katika kipindi cha maonesho.

Karibu utembelee Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ujionee wanyamapori hai kama vile Simba, Chui, Nyati, na ndege wa aina mbalimbali katika mazingira ya kuvutia. 

“Njoo ujionee Wanyamapori hai kukuza Utalii wa ndani”

                           
Imetolewa na:

KATIBU MKUU
Wizara ya Maliasili na Utalii
S.L.P 1315

© 2023 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top