You Are Here: Home » Whats New » TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Maliasili na Utalii inasikitika kuwajulisha kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dr. Hamisi Kigwangalla (Mb.) na wasaidizi wake wamepata ajali leo asubuhi tarehe 04 mwezi Agosti 2018 eneo la Magugu mkoani Manyara wakiwa njiani kurejea Dodoma wakitoka kwenye ziara ya kikazi mkoani Arusha.

Wizara ya Maliasili na Utalii kwa masikitiko makubwa inawajulisha kuwa kufuatia ajali hiyo Afisa habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bwana Hamza Temba amefariki dunia.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dr. Hamisi Kigwangalla (mb.) pamoja na majeruhi wengine walipelekwa kwa helikopta Hospitali ya Mount Meru iliyopo jijini Arusha kwa uchunguzi zaidi.

Mazishi ya Marehemu Hamza Temba yatafanyika kesho tarehe 05/08/2018 saa saba mchana nyumbani kwao Masama wilayani Hai mkoani Kilimanjaro .

Tutawapatia taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya matibabu ya Mheshimiwa Waziri Dr. Hamisi Kigwangalla (Mb.) na majeruhi wengine.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Hamza Temba mahali pema Peponi.

Imetolewa na:
Dorina G. Makaya
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
04/08/2018

 

© 2021 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top