You Are Here: Home » Whats New » SERIKALI YAIPONGEZA TAASISI YA WANYAMAPORI AFRIKA KWA KUSHIRIKI KATIKA UHIFADHI NA KUPAMBANA NA UJAN

SERIKALI YAIPONGEZA TAASISI YA WANYAMAPORI AFRIKA KWA KUSHIRIKI KATIKA UHIFADHI NA KUPAMBANA NA UJAN

Serikali imeipongeza Taasisi ya Wanyamapori Afrika kwa kuunga mkono jitihada za usimamizi wa wanyamapori na kupambana na biashara haramu ya ujangili nchini.

Serikali imeipongeza Taasisi ya Wanyamapori Afrika kwa kuunga mkono jitihada za usimamizi wa wanyamapori na kupambana na biashara haramu ya ujangili nchini.

Hayo yamesemwa Julai 1,2022 jijini Arusha katika hafla ya kusherehekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Taasisi ya Wanyamapori Afrika.

“Tumekuwa tukishirikiana kwa pamoja katika kuendeleza uhifadhi na shughuli za usimamizi wa wanyamapori hasa katika kukomesha biashara haramu ya ujangili ikiwa ni pamoja na kuanzisha vitengo vya mbwa waliopatiwa mafunzo ya hali ya juu kutumika kukagua nyara kwenye viwanja vya ndege vya Kilimanjaro (KIA), Julius Nyerere (JNIA) na katika bustani na vituo vikuu vya usafiri” Mhe. Masanja amesisitiza.

Aidha, amesema taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa viongozi wanaohusika na masuala ya uhifadhi barani Kiafrika na pia kushirikisha jamii katika masuala ya uhifadhi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Masanja ameipongeza taasisi hiyo kwa kuandaa Maonesho ya Tuzo za Wanyamapori za Benjamin Mkapa za Afrika kwa mwaka 2021 yanayoonesha picha bora zaidi za asili zilizopigwa barani Afrika zinazosimulia hadithi ya uhifadhi ya Afrika kwa njia za ubunifu kwa kutumia kamera.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top