You Are Here: Home » Whats New » SERENGETI YAENDELEA KUBAKIA KILELENI KWA UBORA BARANI AFRIKA 2021

SERENGETI YAENDELEA KUBAKIA KILELENI KWA UBORA BARANI AFRIKA 2021

SERENGETI YAENDELEA KUBAKIA KILELENI KWA UBORA  BARANI AFRIKA 2021

Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda Tuzo ya kuwa Hifadhi bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2021. Tuzo hiyo imetangazwa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya mtandao.Hii ni mara ya tatu kwa Serengeti kushinda katika kundi la Hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi Barani Afrika baada ya kushinda tuzo hiyo mwaka 2019 na 2020.

Serengeti imeibuka na ushindi katika shindano hilo lililoshindanisha hifadhi nyingine za Central Kalahari ya Botswana,  Etosha ya Namibia, Kidepo Valley ya Uganda, Kruger ya Afrika Kusini na Maasai Mara ya Kenya.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti yenye ukubwa wa Kilometa za mraba 14,763 inajivunia umaarufu wa kuwa na misafara wa nyumbu wahamao zaidi ya milioni moja na nusu, aina 70 za wanyamapori wakubwa , mimea na spishi mbalimbali za ndege zipatazo 500 zinaopatikana kwa wingi katika hifadhi hiyo, madhari nzuri ya kuvutia pamoja na shughuli mbalimbali za utalii zinazovutia watalii wengi.

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) linaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi, Wadau wa Utalii pamoja na wote waliotumia muda wao kupiga kura na kuifanya Serengeti kuwa mshindi wa Hifadhi Bora zaidi kwa Bara la Afrika kwa mara ya tatu mwaka 2021.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top