You Are Here: Home » Whats New » NCHI WANACHAMA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ZASEMA ZIKO TAYARI KUPOKEA WATALII

NCHI WANACHAMA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ZASEMA ZIKO TAYARI KUPOKEA WATALII

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimesema kuwa ziko tayari kupokea wageni wa utalii kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi hizo. Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki wakati wa ufunguzi wa Onesho la Kwanza la Utalii la jumuiya ya Afrika Mashariki.

‘’Nchi zetu za Afrika mashariki zimebarikiwa kuwa na vivutio vizuri na vya kila aina ukija Tanzania kuna mlima Kilimanjaro, hifadhi nzuri ya Serengeti ukienda kenya utaona Masai mara ukienda Burundi,Rwanda ,Sudan na Uganda kuna milima mizuri na mandhari ya kipekee ya utalii’’

Amesema pamoja na kwamba kulikuwa na mlipuko wa COVID-19 ambao ulichangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa sekta utalii lakini nchi zetu zimejipanga kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inaimarika.

‘’Tunajua kabla ya ugonjwa wa COVID-19 , mwaka 2019 tulipokea idadi ya watalii milioni saba Afrika Mashariki lakini tulitegemea 2025 kupokea watalii milioni kumi na tano ’’

Kwa upande wake , Waziri wa Maliasili na Utali, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Julai mwaka huu , Jumuiya ya Afrika Mashariki ilipitisha Mkakati na mpango wa kuutangaza utalii kwa pamoja lengo likiwa ni kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya utalii.

Dkt. Ndumbaro amesema kupitia mpango huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuzaa onesho la utalii kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki huku Tanzania ikipata bahati ya kipekee ya kuandaa onesho hilo

‘’Ni heshima kubwa kwa Tanzania na kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan’’ amesema Dkt. Ndumbtano

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top