You Are Here: Home » Whats New » NAIBU WAZIRI MASANJA AIPONGEZA SERIKALI KWA KUKUSANYA MAPATO KATIKA MFUKO MKUU WA SERIKALI

NAIBU WAZIRI MASANJA AIPONGEZA SERIKALI KWA KUKUSANYA MAPATO KATIKA MFUKO MKUU WA SERIKALI

NAIBU WAZIRI MASANJA AIPONGEZA SERIKALI KWA KUKUSANYA MAPATO KATIKA MFUKO MKUU WA SERIKALI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameipongeza Serikali kwa kutekeleza takwa la kisheria la kuhakikisha makusanyo yote yanaingia kwenye kapu moja (Mfuko Mkuu wa Serikali) kwa kubadili Sheria ya Fedha ya mwaka 2020 (Finance Act 2020) ambapo jukumu la kukusanya mapato yasiyo ya kodi ikiwemo ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) lilikasimiwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Ameyasema hayo leo Bungeni jijni Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Malinyi, Mhe. Antipas Zeno Mgungusi kuhusu Serikali kurekebisha utaratibu wa kuwaachia makusanyo ya fedha Jeshi la Uhifadhi hasa TANAPA.

Amefafanua kuwa katika kipindi cha mwaka 2019/2020 mapato ya Jeshi la Uhifadhi (TANAPA) yalishuka kutokana na kushuka kwa ukusanyaji wa mapato ya TANAPA ulishuka kutokana na kupungua kwa wageni kufuatia makatazo ya kusafiri na kufungiwa (lockdown) baada ya kuibuka kwa janga la UVIKO-19”

Mhe. Masanja ameeleza kuwa hali hiyo ilisababisha Jeshi la Uhifadhi (TANAPA) kushindwa kumudu gharama mbalimbali za uendeshaji na kutokana na changamoto hizo za kimapato, Serikali iliamua kugharamia shughuli zote za uhifadhi ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi na kutoa ruzuku ya kugharamia matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo.

Wakati huohuo, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka kuhusu Serikali kutumia mbao za mitiki ambayo ina ubora sawa na Mninga na Mkongo katika utengenezaji wa samani za Mhe. Masanja amesema kutokana na utafiti uliofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii, kuzingatia Serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza miti mipya iliyofanyiwa utafiti katika orodha ya miti iliyoainishwa katika Sheria ya manunuzi inayosimamiwa na PPRA ili itumike katika kutengeneza samani za Serikali.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top