You Are Here: Home » Whats New » NAIBU WAZIRI KANYASU AHAMASISHA UFUGAJI NYUKI KIBIASHARA

NAIBU WAZIRI KANYASU AHAMASISHA UFUGAJI NYUKI KIBIASHARA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ametoa hamasha kwa wakazi Kisiwa cha Ukerewe kilichopo mkoani Mwanza kutambua umuhimu wa kufuga nyuki na faida ya asali kiuchumi na kiafya.

Aidha, Mhe.Kanyasu ametoa ruhusa kwa wananchi wenye nia ya kufuga nyuki kuitumia misitu ya Hifadhi mitano iliyopo katika Kisiwa hicho inayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya hiyo kutundika mizinga yao katika misitu hiyo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ametoa hamasha kwa wakazi Kisiwa cha Ukerewe kilichopo mkoani Mwanza kutambua umuhimu wa kufuga nyuki na faida ya asali kiuchumi na kiafya.

Aidha, Mhe.Kanyasu ametoa ruhusa kwa wananchi wenye nia ya kufuga nyuki kuitumia misitu ya Hifadhi mitano iliyopo katika Kisiwa hicho inayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya hiyo kutundika mizinga yao katika misitu hiyo.

Mhe. Kanyasu ametoa ruhusa hiyo kutokana idadi kubwa ya watu katika Kisiwa hicho huku kukiwa na ufinyu wa ardhi unaokikumba kisiwa hicho.

Mhe.Kanyasu amesema lengo ni kuwasaidia wananchi kubadili mfumo wa maisha kwa kuanza kufuga nyuki kibiashara badala ya kulima na kuvua samaki pekee.

Akizungumza na Kikundi cha Walemavu wanaojishughulisha na useremala wa kutengeneza mizinga ya nyuki ya kisasa mjini Nansio Ukerewe, Naibu Waziri amesema misitu hiyo mitano yenye jumla ya zaidi ya hekta 1300 itawasaidia kuitumia kufuga nyuki kibiashara.


Amesema kutokana na ongezeko kubwa la watu wapatao zaidi 400,000 katika Kisiwa hicho chenye ukubwa usiozidi kilomita za mraba 700 ambalo ni eneo la nchi kavu , Wakazi wa Kisiwa hicho wana kila sababu ya kujiingiza kufuga nyuki.


Hata hivyo, Mhe.Kanyasu amewaambia wananchi hao kuwa kutokana na ardhi ya kilimo kuchoka pamoja na kupungua kwa samaki kutokana na kukithiri kwa uvuvi haramu njia mbadala ni kufuga nyuki kutokana na mahitaji makubwa ya asali ndani na nje ya nchi.


Amewahakikishia uwepo wa soko la uhakika kutokana na mahitaji makubwa ya asali katika nchi ya China na Marekani, Amesema hata hivyo Tanzania bado haijaweza kukidhi mahitaji ya soko hilo.


Amesema China pekee inahitaji asali tani 600,000 kutokana na uzalishaji duni Tanzania bado haijaweza kusafirisha hata nusu tani ya asali hiyo inayohitajika.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa wilaya Halmashauri hiyo, Esther Chaula ameahidi kutoa mkopo kwa kikundi hicho cha Walemavu   ili waweze kutengeneza mizinga mingi itakayorahisisha upatikaji wa mizinga ya kutosha kwa ajili ya kufugia nyuki.


Ameongeza kuwa ufugaji wa nyuki katika misitu hiyo ya TFS itatoa ahueni ya ulinzi shirikishi kwa vile wananchi wataona faida ya moja kwa moja kupitia asali wanayoipata.


Katika hatua nyingine Mhe. Kanyasu ameiagiza TFS ihakikishe inanunua mavazi maalum ya kulinia asali na kuyasambaza katika vituo vyao ambayo wananchi watakuwa wakiyaazima wakati wa kurina asali badala ya wananchi hao kuendelea kutumia moto wakati wa kulina asali


Amesema takribani nyuki bilioni moja kila mwaka huuawa kwa moto kutokana na urinaji huo ambao sio rafiki wa mazingira.


Awali,  Kiongozi wa kikundi Walemavu hao, Nestory Kilampa alimueleza Naibu Waziri huyo kuwa licha ya kutengeneza mizinga hiyo soko lake limekuwa la kusuasua kutokana na hamasa ndogo kutoka kwa wananchi juu ya umuhimu wa kufuga nyuki kibiashara.


” Tunaamini ujio wako hapa utatoa hamasa kwa wananchi kugeukia fursa ya kufuga nyuki na kuachana shughuli za uvuvi pamoja na kilimo cha mazoea na badala yake watajikita kufuga nyuki ili kujiingizia kipato.

© 2020 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top