You Are Here: Home » Whats New » NAIBU KATIBU MKUU AKAGUA UTEKELEZAJI MIRADI YA REGROW

NAIBU KATIBU MKUU AKAGUA UTEKELEZAJI MIRADI YA REGROW

NAIBU KATIBU MKUU AKAGUA UTEKELEZAJI MIRADI YA REGROW

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi amefanya ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya kuwanufaisha wananchi kiuchumi na uendelezaji Utalii inayotekelezwa chini ya mradi wa REGROW katika eneo la Madibira wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Miongoni mwa miradi aliyoitembelea ni pamoja na Skimu ya umwagiliaji inayotumiwa na wakulima wa Kata ya Madibira wilayani Mbarali pamoja alama za mipaka katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Naibu Katibu Mkuu amepongeza juhudi mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kuhakikisha wananchi waliokusudiwa katika mradi huo wanaendelea kunufaika pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi kwa kulinda maeneo ya hifadhi yanayowazunguka.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top