You Are Here: Home » Whats New » *MISITU YAAJIRI WATU ZAIDI YA MILIONI 4* .

*MISITU YAAJIRI WATU ZAIDI YA MILIONI 4* .

*MISITU YAAJIRI WATU ZAIDI YA MILIONI 4* .


Kufuatia Sekta ya Misitu kuzalisha ajira zaidi ya milioni 4 nchini wito umetolewa kwa sekta hiyo iendelee kupewa kipaumbele katika uhifadhi ili iongeze mchango zaidi katika Pato la Taifa.

Kufuatia Sekta ya Misitu kuzalisha ajira zaidi ya milioni 4 nchini wito umetolewa kwa sekta hiyo iendelee kupewa kipaumbele katika uhifadhi ili iongeze mchango zaidi katika Pato la Taifa.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokutana na uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.

“Naipongeza TFS kwa kusimamia vyema watumishi na kuendesha taasisi kwa kutumia mifumo ya kielekroniki, utendaji huo umepelekea TFS kuibuka mshindi kati ya taasisi za umma katika usimamizi wa rasilimali watu mwaka 2021 na pia mshindi wa kwanza kati ya Wizara na taasisi za umma kwa kuwa na mifumo mizuri ya ufuatiliaji na tathmini (M&E) kwa mwaka 2021/2022”. Alisema Waziri Chana

Licha ya kuipongeza TFS kwa kazi na mikakati mizuri iliyowekwa, Waziri Chana amesema kuwa atahakikisha anatembelea maeneo yote yenye hifadhi za Misitu ili kujionea uhalisia wa yale yaliyowasilishwa kwenye Taarifa aliyopatiwa.

Kwa upande wake Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akizungumza wakati wa kikao hicho ameeleza kuwa baadhi changamoto wazokabiliana nazo ni uvamizi wa misitu kwa shughuli za Kilimo cha kuhamahama, makazi na uchungaji mifugo.

“Changamoto nyingine ni pamoja na kushambuliwa kwa maafisa na askari wa Jeshi la Uhifadhi kitengo cha Misitu wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya uhifadhi, moto pori na uvunaji holela wa mazao ya misitu hususani kwenye ardhi za vijiji”. Alifafanua Prof Silayo

Adha, katika kuhakikisha sekta ya misitu inakua endelevu hapa nchini Prof. Silayo amesema taasisi yake imeandaa Mkakati wa miaka 30 ya usimamizi na uendelezaji mashamba ya miti ya Serikali ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu hapa nchini.

“Sehemu ya makakati huo ni kuongeza eneo la upandaji miti kutoka wastani wa hekta 120,000 hadi 170,000 ifikapo mwaka 2025.

Aidha, TFS inakamilisha mradi wa bustani ya miche ya miti itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha miche zaidi ya milioni 2.6 kwa mara moja jijini Dodoma” alisema Prof Silayo.

Prof. Silayo aliongeza kuwa TFS inaendelea kuongeza jitihada za kushirikisha jamii na taasisi za umma na binafsi katika upandaji miti, alitaja jitihada hizo kuwa ni pamoja na mpango mahususi wa kupanda na kuboresha mandhari za shule maarufu kama “eco schools” ulioanza kutekelezwa katika maeneo ya nyanda kame.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top