You Are Here: Home » Whats New » MAWAZIRI WAKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI BWAWA LA UMEME LA JULIUS NYERERE, WAPONGEZA

MAWAZIRI WAKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI BWAWA LA UMEME LA JULIUS NYERERE, WAPONGEZA

MAWAZIRI WAKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI BWAWA LA UMEME LA  JULIUS NYERERE, WAPONGEZA

Mawaziri kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere unaotarajiwa kukamilika mwakani ambapo wamepongeza kazi kubwa inayoendelea kufanyika.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua zoezi la ung’oaji miti unaofanywa na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wA Tanzania (JWTZ) katika eneo linalotarajiwa kuchimbwa Bwawa kwa ajili ya kufua Umeme wa maji lililoko katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere mkoani Morogoro

Akizungumza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema lengo la ziara hiyo ni   kuangalia zoezi la kung’oa miti na usafishaji eneo ambalo kutakuwa na bwawa, Kazi ambayo Wizara ya Maliasili na Utalii imepewa jukumu ya kulisimamia.

Katika ziara hiyo mbali ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro pamoja Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamaed Mchengerwa kushiriki, Pia ziara hiyo iliambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki.

Akizungumza na mara baada ya kukagua eneo ambalo Bwawa linatajiwa kujengwa, Waziri, Dkt. Ndumbaro amewataka Wafanyakazi walioaminiwa kufanya kazi katik amradi huo kufanya kazi kwa bidii kwa kutanguliza mbele uzalendo .


Amesema kukamilikwa kwa mradhi huo unaotarajiwa kuzalisha Umeme wa Megawati 2115 utakuwa ni ushindi mkubwa Taifa kwa vile tokea mwanzo umekuwa ukipigwa vita kali kutoka ndani nanje ya nchi kwa kisingizio kuwa unachangia kuharibu mazingira.

“Watu wengi wakiangalia bwawa hili wanaona liko kwenye Wizara Moja ya Nishati lakini bwawa hili linagusa Wizara nyingi sana ,Moja inagusa Wizara ya Maji lakini pili inagusa Wizara ya Mazingira kwasababu lazima tuyatunze hayo Mazingira Ili tuyapate hayo maji na tatu inagusa Wizara ya Maliasili na Utalii ndio yenye misitu ambayo inatunza Mazingira, lakini hapa panapo jengwa hii ni hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere kwahiyo ujenzi huu unagusa Sekta nyingi” Dkt Ndumbaro Amesema

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema dhamira yao kubwa ya kutembelea mradi huo ni kuwatia Moyo makamanda ambao wanatekeleza mradi huo.

” Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema ziara hiyo ili kuangalia changamoto zinaweza kuwachelewesha ambazo zinaweza kutatuliwa na Viongozi wa Wizara hizo mbilki na hata kama Wizara nyingine lengo likiwa ni kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mary Masanja amesema kuwa kwa sasa hivi Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba maeneo ambayo tayari yatakuwa yameathirika na ukataji miti yataanza kupandwa ili kuweza kulinda vyanzo vya maji.

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kulihifadhi eneo hilo la mradi kwa kupanmda miti asili ili kuhakiisha Bwawa hilo linakuwa kivutio kingine cha Utalii.

‘’ Tumekagua eneo hili licha ya kuwa litatumika kuzalisha Umeme pia litakuwa ni eneo zuri la kiutalii kulingana na madhari yake hivyo tuanategemea Watalii watakaokuja kuangalia wanyamapori hawataishia kuona wanyamapori bali wataona na mradi huu pia.

© 2021 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top