You Are Here: Home » Whats New » MAKAMU WA RAIS WA UGANDA MHE JESSICA ALUPO ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA

MAKAMU WA RAIS WA UGANDA MHE JESSICA ALUPO ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA

MAKAMU WA RAIS WA UGANDA MHE JESSICA ALUPO ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA

Makamu wa Rais wa Uganda Mhe. Jessica Alupo ametembelea Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea na Urithi adhimu na adimu wa Historia ya Tanzania uliohifadhiwa katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

Mhe. Alupo alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga, na kupatiwa maelezo ya Uhifadhi wa Uridhi wa Utamaduni na Historia kutoka kwa Wataalam wa Makumbusho hiyo.

Mhe .Jessca Alupo alikuja nchini kuhudhuria Mkutano wa Wanawake na Vijana katika biashara chini ya Mkataba wa Eneo huru la biashara Afrika uliofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa Uganda ni miongoni mwa nchi za Bara la Afrika ambazo huleta watalii wengi nchini Tanzania takribani 21,080 waliongia nchini kuanzia mwezi Januari hadi Julai, 2022 ikishika nafasi ya nne baada ya Kenya, Burundi na Malawi.

© 2023 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top