You Are Here: Home » Whats New » MAFANIKIO NA MAENDELEO YA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA UHURU

MAFANIKIO NA MAENDELEO YA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA UHURU

MAFANIKIO NA MAENDELEO YA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA UHURU

UTANGULIZI

Ndugu Wanahabari,

Tanzania imejaaliwa kuwa na maeneo ya hifadhi za wanyamapori, misitu na nyuki; na malikale yenye mchango mkubwa katika uhifadhi wa mazingira, ustawi wa wananchi na ukuaji wa uchumi. Mchango huo unatokana na uhifadhi wa mifumo ikolojia unaokidhi matakwa ya kimazingira, kijamii na kiutamaduni, kitaifa, kikanda na kimataifa. Aidha, maeneo ya maliasili yanatoa huduma za maji kwa matumizi mbalimbali; makazi ya wanyamapori na viumbe wengine, uchavushaji, uhifadhi wa udongo, ufyonzaji wa hewa ukaa (carbon) na hivyo kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kiuchumi, maliasili na malikale zimeendelea kuchangia katika kuingiza fedha za kigeni na Pato la Taifa (GDP) kupitia utalii, ajira, nishati, elimu, utafiti, utamaduni, burudani na tiba. Mfano sekta ya utalii huchangia takriban asilimia 25 ya fedha za kigeni na zaidi ya asilimia 17 katika Pato la Taifa. Aidha, ustawi wa sekta ndogo ya utalii unategemea pamoja na masuala mengine, uhifadhi mzuri wa maliasili, malikale, historia na utamaduni. Uhusiano bora kati ya uhifadhi na maendeleo unachangia katika ustawi wa maliasili, matumizi endelevu, ustawi wa wananchi na ukuaji wa uchumi.

Kwa kuzingatia mgawanyo wa mamlaka nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imepewa dhamana ya kusimamia uhifadhi wa maliasili, malikale na maendeleo ya utalii. Wizara inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni, mipango ya maendeleo na maelekezo mbalimbali ya Serikali.

MAFANIKIO YA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Ndugu Wanahabari,
Katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, Serikali kupitia Sekta ya Maliasili, Malikale na Utalii imeliwezesha Taifa kupata mafanikio mbalimbali kama ifuatavyo:-


2.1 SEKTA YA UTALII

2.1.1 Kukua na kuimarika kwa shughuli za utalii

Sekta ya utalii ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania. Katika miaka 60 iliyopita Serikali iliimarisha utalii nchini kwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa mikakati ya kukuza vivutio mbalimbali vya utalii vikiwemo hifadhi za wanyamapori, maporomoko ya maji, milima, misitu ya mazingira asilia, utamaduni, fukwe na malikale.

Kupitia uendelezaji wa vivutio hivyo, Tanzania imeweza kupata mafanikio mbalimbali yakiwemo:-

2.1.2 Kuongezeka kwa idadi ya Watalii na Mapato

Kutokana na juhudi za Serikali za kuendeleza na kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii nchini, idadi ya Watalii wanaoingia nchini kutoka katika nchi mbalimbali Duniani imeongezeka kutoka 9,847 Mwaka 1960 hadi kufikia watalii 1,527,230 Mwaka 2019. Kadhalika, kumekuwepo na ongezeko la mapato yatokanayo na watalii, kwa mfano mwaka 1995 mapato yalikuwa Dola za Marekani milioni 259.44 ambapo yaliendelea kuongezeka hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.6 mwaka 2019 kabla ya Ugonjwa wa UVIKO-19. Kutokana na jitihada za Serikali katika kukabliliana na ugonjwa wa UVIKO-19 idadi ya watalii imeanza kuongezeka kutoka watalii 620.867 mwaka 2020 hadi kufikia 716,169 mwezi Oktoba 2021. 

2.1.3 Kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi katika shughuli za utalii

Serikali imefanikiwa kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii katika kutangaza na kuhamasisha utalii wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo, watu wenye mahitaji maalum, vikundi vya kidini, Madereva wa bodaboda na bajaji, mashirika binafsi na ya kiserikali. Aidha, wananchi wengi wemeendelea kushiriki kwenye shughuli za utalii ambapo ajira takriban milioni 1.6 za moja kwa moja na zile ambazo sio za moja zimepatikana.

Aidha, katika kuendelea kujenga mazingira bora ya kuwawezesha wananchi hususan vijana kuanzisha biashara za utalii nchini, Serikali imepunguza viwango vya ada ya leseni kutoka Shilingi za Tanzania sawa na Dola za Marekani 2000 hadi Shilingi za Tanzania sawa na Dola za Marekani 500 kwa magari kuanzia moja hadi matatu. Hatua hii imelenga kuongeza ushiriki wa wakala wa biashara za utalii ambao ni wazawa katika biashara za utalii. Kufuatia hatua hiyo, wakala wa biashara za utalii wazawa waliongezeka kutoka wakala 643 hadi kufikia 1,687 sawa na ongezeko la asilimia 162.4.

2.1.4 Kuongezeka kwa juhudi za kutangaza utalii ndani na nje ya nchi

Katika kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi,. Serikali imeendelea kubuni na kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kuandaa na kushiriki kwenye makongamano, maonesho na ziara za utangazaji utalii (exhibition and road shows) katika masoko ya msingi (Uingereza, Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Hispania na Australia) na masoko ya kimkakati (China, Urusi, India, Poland, Jamhuri ya Czech, Israeli, Uturuki, Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait na Saudi Arabia); kuimarisha matumizi ya TEHAMA; kuandaa ziara za mfunzo kwa waandishi wahabari wa kimataifa, mawakala wa ulii, na mawakala wa Usafirishaji kwa ajili ya kusaidia kutangaza Utalii wa Nchi yetu.
Aidha, Wizara imeendelea kutumia ofisi za Balozi za Tanzania nje ya nchi Kimkakati kutangaza na kuhamasisha utalii kikanda na kimataifa; kutumia mabalozi wa hiari (goodwill ambassadors) kutangaza Utalii; na kutumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi katika kutangaza na kuhamasisha utalii.

Kupitia juhudi hizi vivutio vya utalii vya Tanzania vimepata umaarufu mkubwa na Tuzo mbalimbali za Kimataifa. Mfano ni Hifadhi ya Taifa Serengeti kuwa hifadhi Bora zaidi

PRESS_-_MIAKA_60_YA_UHURU_%282%29_final_dpp_30_nov_2021_%281%29

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top