You Are Here: Home » Whats New » MABADILIKO YA MANAIBU MAKAMISHNA WA UHIFADHI WA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO

MABADILIKO YA MANAIBU MAKAMISHNA WA UHIFADHI WA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO

MABADILIKO YA MANAIBU MAKAMISHNA WA UHIFADHI WA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

                                                     

MABADILIKO YA MANAIBU MAKAMISHNA WA UHIFADHI WA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb), kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Sura Na. 284, leo tarehe 19 Disemba, 2020 amefanya mabadiliko ya Manaibu Makamishna wa Uhifadhi wawili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hii.

Katika mabadiliko hayo, Mhe Waziri amemteua Dkt. Christopher D. Timbuka, kuwa Kaimu Naibu Kamishna (Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii). Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Timbuka alikuwa Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Kanda ya Kusini. Anachukua nafasi ya Bw. Ephraim A. Mwangomo ambaye amerejeshwa TANAPA.

Aidha,  Mhe Waziri amemteua Bw. Audax R. Bahweitima, kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Huduma za Shirika). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Bahweitima alikuwa Mchumi Mkuu katika Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii. Anachukua nafasi ya Bw. Abdallah O. Kiwango ambaye amerejeshwa TANAPA.

© 2021 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top