You Are Here: Home » Whats New » MIFUGO YA WANANCHI NA MALI ZAO IMEWASILI SALAMA MSOMERA

MIFUGO YA WANANCHI NA MALI ZAO IMEWASILI SALAMA MSOMERA

MIFUGO YA WANANCHI NA MALI ZAO IMEWASILI SALAMA MSOMERA

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana amewapongeza waratibu wote na wananchi wa Ngorogoro walioamua kuhamia kijiji Cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni Tanga, kwa kuratibu vizuri zoezi la kuhamisha watu na mifugo.

Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana ameyasema hayo kijiijini Msomera Tanga mara baada ya kujihakikishia kuwa mifugo ya wafugaji hao waliohama kwa hiyari yao kutoka hifadhi ya Ngorogoro imefika salama.

“Tunamshuku Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu wetu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri Mkuu wetu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kutuongoza vyema kwenye jambo hili, limeenda vizuri na linaenda vizuri kwa wanangorogoro wenyewe kuhama kwa hiyari, sisi kama Wizara tutaendela kutekeleza maagizo ya Viongozi wetu wa juu ili kuhakikisha ndugu zetu wanaishi kwenye Mazingira Bora kama mlivyo yaona”. Amesema Waziri Chana

Akizungumzia hali ya Usalama ya wafugaji hao, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima amesema wananchi hao wapo salama na wataendelea kuwa salama wao na mifugo yao hivyo Serikali ya Mkoa imejipanga vyema kuwahudumia vizuri kwa kuwa wamesha kuwa wakazi wa Tanga.

Naye Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso amesema miradi ya maji imeshafanyika na wanaendelea kuhakikisha kuwa hakuna changamoto yeyote ya maji kwa Matumizi ya binadamu na kunywesha mifugo iliyofika na itakayo fika.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top