You Are Here: Home » Whats New » KAMATI YA BUNGE YAVUTIWA NA MRADI WA REGROW,  YATAKA UKAMILIKE KWA WAKATI

KAMATI YA BUNGE YAVUTIWA NA MRADI WA REGROW,  YATAKA UKAMILIKE KWA WAKATI

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeonesha kuvutiwa na utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW wakitoa wito kwa mradi huo kukamilika kwa wakati ili wananchi wa Kusini waanze kunufaika kupitia vivutio vya utalii walivyonavyo

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeonesha kuvutiwa na utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW wakitoa wito kwa mradi huo kukamilika kwa wakati ili wananchi wa Kusini waanze kunufaika kupitia vivutio vya utalii walivyonavyo

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na Wajumbe wa Kamati hiyo mara baada ya Mratibu wa mradi huo, Dkt. Aenea Sanya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mradi huo leo Jijini Dodoma.

Akizungumzia mradi huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.  Juma Ally Makoa amesema mradi huo wenye lengo la kuongeza ubora wa vivutio vya utalii katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania utakuwa chachu ya kuwavutia watalii wengi waliokuwa wanakwenda Kaskazini kuanza kutembelea vivutio vilivyo ukanda wa mikoa ya kusini kwa kuwa maeneo hayo yataanza kufikika kwa urahisi.

Sambamba na hilo Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Hawa Mwaifunga ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo amesema licha ya mradi huo kuwa katika hatua mbalimbbali za utekelezaji tayari umeanza kuwagusa kiuchumi wananchi wanaozunguka hifadhi za kipaumbele

Amesema mradi huo umeanza kuboresha miundombinu ya umwagiliaji ambapo jumla wakulima zaidi 40,000 wameanza kunufaika na utekelezaji huo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi amewaeleza Wajumbe hao kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa kuzingatia muda uliopangwa ili uweze kuleta matokeo chanya kwa Watanzania

‘’ Tumedhamiria kufungua vivutio vya Kusini ili watalii wetu waweze kuwa na chaguo la maeneo mengi ya kwenda kufurahi vivutio vya Utalii tulionao ndani ya nchi yetu’ Amesisitiza Mkomi

Mradi wa REGROW unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa thamani ya Dola za Kimarekani milioni 150 (sawa na TZS 345 Bilioni), ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia. Mradi huo ulianza rasmi mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2025

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top