You Are Here: Home » Whats New » KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA MALIASILI NA UTALII

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA MALIASILI NA UTALII

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA MALIASILI NA UTALII

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kazi nzuri ya Uhifadhi wa Maliasili na uendelezaji wa Utalii hapa nchini.

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe. Juma Ally Makoa (Mb) wakati wa kikao cha Kamati hiyo na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mhe. Makoa amesema Kamati yake inaridhishwa na kutiwa moyo na juhudi kubwa zinazofanywa na Wizara katika kulinda wanyamapori waliokuwa hatarini kutoweka hususan Faru kutokana na idadi yao kuongezeka.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana licha ya kuishukuru Kamati hiyo kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa kwa Wizara amesema Wizara anayoiongoza itaendelea kuufanyia kazi ushauri unaotolewa na Kamati hiyo ili kuendeleza sekta hiyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top