You Are Here: Home » Whats New » IDARA YA UTALII YATAKIWA KUKUTANA NA WADAU WA UTALII

IDARA YA UTALII YATAKIWA KUKUTANA NA WADAU WA UTALII

Idara ya Utalii nchini imetakiwa kukutana na wadau wa Utalii kwa lengo la kuhakikisha wadau hao wanaendana na kasi ya ujio mkubwa wa watalii ambao ni matokeo chanya ya Filamu ya Royal Tour.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana alipokutana na Uongozi wa Idara hiyo Ofini kwake Jijini Dodoma.

Waziri Chana amesema licha ya changamoto kadhaa zinazoikabili Idara hiyo, lakini imejitahidi kukabiliana nazo na hivyo inastahili pongezi kwa juhudu za kuongeza mapato.

Awali akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Idara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii nchini Bw Philip Chitaunga ametaja moja ya mafanikio ni pamoja na kukusanya maduhuli ya Serikali kutoka kwa wakala wa utalii kiasi cha Tsh 6,437,011,2503 ikiwa ni 86.9% ya lengo la Bilioni 7.4.

Licha ya Mafanikio makubwa ya Idara hiyo Bw Chitaunga amezitaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na ubovu wa miundombinu, kutokuwa na mawasiliano ya Simu kwenye maeneo mengi ya Utalii, Vita vya Ukraine na Urusi nk.

© 2022 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top