You Are Here: Home » Whats New » AFRIKA KUWA NA KAULI MOJA BIASHARA YA UWINDAJI WA KITALII

AFRIKA KUWA NA KAULI MOJA BIASHARA YA UWINDAJI WA KITALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amezitaka nchi za Afrika kuwa na kauli moja kuhusu taratibu na bei za wanyamapori katika biashara uwindaji wa kiutalii

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao ana kwa ana na baadhi ya mawaziri wa Utalii wa nchi za Afrika katika Mkutano wa 64 wa Kimataifa wa Utalii uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii Duniani (INWTO) unaofanyika kwa muda wa siku nne nchini Cape Verde.


Amesema bei za wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa pamoja na vitalu vya uwindaji wa Wanyamapori zimekuwa zikitofautiana sana kati ya nchi na hali hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa shughuli uhifadhi barani Afrika.


Akizungumza katika vikao hivyo vya ana kwa ana na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe.Mhe.Ngobhithize Ndlovu amezitaka nchi hizo kuwa kitu kimoja katika kuamua na kupanga bei za uwindaji wa Kitalii.


Amesema kutokana na kutofautiana kwa bei na baadhi ya kanuni na taratibu hizo Wawindaji wa kiitalii wamekuwa wakitumia mwanya huo kuzikandamiza nchi za Kiafrika kwa kupanga bei wanazotaka wao huku wakidai kuwa bei hizo cha chini zimekuwa katika nchi nyingine pia.


Amesema Wawindaji hao wamekuwa wakipanga bei za uwindaji wa kiutalii na sio nchi husika huku wakidai kuwa kama bei hiyo haitawezekana basi watakwenda katika nchi nyingine ambayo utalii wake uwindaji ni bei ya chini zaidi


” Utofauti wetu huu umekuwa ukitukandamiza kama nchi kwani tulitakiwa sisi ndo tupange bei lakini kutokana na kutokuwa na umoja bei za wanyama zimekuwa zimekuwa zikiamuliwa na wao hili lazima tulikatae kwa kuungana kwa pamoja ” alisisitiza Dkt.Ndumbaro


Kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro amezitaka nchi zote zinazoendesha utalii wa uwindaji zifanye mkutano kwa nji ya mtandao ili kujadili mustakabali wa biashara hiyo na kisha zitoke na kauli moja ili kuwathibiti wawindaji wa kitalii kwa ajili ya maslahi mapana ya uhifadhi barani Afrika.
Amezitaja baadhi ya nchi wanachama wa SADC zinazofanya vizuri katika uwindaji wa kitalii kuwa ni Botswana, Zimbabwe pamoja, Zambia na Afrika ya Kusini

Katika hatua nyingine , Dkt.Ndumbaro ametoa ahadi kwa nchi ya Zimbabwe kama itakuwa tayari ipewe mafunzo ya kuendesha biashara ya uwindaji wa kiutalii kwa mfumo wa kidigitali ambao utasaidia kuongeza mapato maradufu


Amesema tangu kuanzisha kwa mfumo huo nchini Tanzania umeleta manufaa makubwa kwa nchi ambapo Wawindaji wa kitalii ili kuweza kupata vitalu vya uwindaji wamekuwa wakilazika kushiriki katika mnada wa kimtandao.


Naye, Waziri waUtalii wa ZimbabweMhe.Ngobhitithize Ndlovu amesema nchi za kiafrika lazima ziungane katika suala hilo kwani katika nchi ya Zimbabwe Wawindaji hao pia wamekuwa wakipanga bei huku wakidai kama hiyo bei haitawezekana watakwenda Tanzania ambako bei vitalu vya uwindaji ipo chini zaidi


Amesisitiza kuwa shughuli za uhifadhi zimekuwa aghali sana huku biashara hiyo ya uwindaji wa kiutalii ukibaki pale pale kutokana na kutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine


Naye, Kamishna Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi amesema umoja huo wa nchi za Kiafrika katika biashara ya vitalu vya uwindaji italiingizia taifa fedha nyingi za kigeni sio kwa Tanzania pekee bali kwa Afrika nzima


” Biashara hiyo imekuwa na ushindani baina yetu bila kujuana kufuatia kila nchi kupanga bei zake kulingana na matakwa ya wadau hao huku shughuli za uhifadhi zikiwa juu zaidi” amesisitiza Kamishna Mabula.

© 2021 - Ministry of Natural Resources and Tourism Tanzania

Scroll To Top