Whats New
Oct
2022
NAIBU KATIBU MKUU JUMA MKOMI ATOA WITO KWA WABUNGE KULINDA RASILIMALI ZA MALIKALE.
Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi ametoa wito kwa Wabunge kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuyalinda na kuyatunza maeneo ya Malikale kwani ni rasilimali isiyorejesheka pale inapoharibiwa.
Read More
Oct
2022
WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUDHIBITI MOTO KWENYE MASHAMBA YA MITI
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja(Mb) amewataka wananchi Mkoani Iringa kushirikiana katika kudhibiti matukio ya moto yanayojitokeza kwenye mashamba ya miti binafsi na ya Serikali. Read More
Oct
2022
WANANCHI SONGWE WATAKIWA KUACHA KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewaasa wananchi wa Kitongoji cha Nkanka ,Kijiji cha Itumba katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, kuacha kuvamia maeneo ya hifadhi hasa katika eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ileje Range. Read More
Oct
2022
WAZIRI BALOZI DKT.PINDI CHANA ASHIRIKI KIKAO CHA DHARURA CHA MAWAZIRI WA SADC
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana leo Oktoba, 25, 2022 ameshiriki kikao cha dharura kwa njia ya mtandao cha Mawaziri wa Maliasili, Mazingira na Utalii wa nchi Wanachama wa Jumuiya Maendeleo ya Kiuchumi ya Kusini mwa Afrika (SADC)
Read More
Oct
2022
WAZIRI DKT. CHANA AMSHUKURU RAIS MHE. SAMIA KWA FEDHA ZA UVIKO-19
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuipatia Wizara ya Maliasili na Utalii kiasi cha Shilingi Bilioni 90.2 zilizotumika kwa ajili ya kuboresha huduma na miundombinu ya utalii… Read More
Oct
2022
WIZARA YAAHIDI KUONGEZA NGUVU KATIKA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) ameiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuwa Wizara anayoiongoza inaendelea kuongeza nguvu katika kutangaza utalii na vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia maonesho na mikutano mikubwa ya Kimataifa… Read More
Oct
2022
MOTO UNAENDELEA KUDHIBITIWA MLIMA KILIMANJARO
Ndugu wananchi,
Tarehe 21 Oktoba, 2022 majira ya saa 2.30 usiku baadhi ya maeneo ya Hifadhi yetu ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro yaliwaka moto uliokuwa ukitokea eneo la Karanga kuelekea Baranco. Juhudi za kuuzima moto huo zilianza mara moja zikihusisha vyombo vya ulinzi… Read More
